Msanii Otile Brown ameanza mambo ya kibongo bongo yanaofanywa na staa mmoja wa Wcb Wasafi ambaye ndiye boss wa timu hio ya usafini Diamond Platumuz.

Otile

Otile akiwa studioni Radio Maisha kutambulisha ngoma ayke ‘Ndogo’ kama alivyoiita mwenyewe  kutokana na hali iliyomsababisha kuiachia kipindi cha uchaguzi nchini kenya ilmradi awape burudani mashabiki wake kipindi hicho ambacho wasanii wengi huogopa kuachia nyimbo zao wa kuhofia kutofanya vizuri wala kopekelewa vizuri kutokana na upepo wa siasa na uchaguzi.

Mkali huyo wa ‘Kistaarabu’ alitambulisha wimbo wake huo mdogo kwa jina ‘Acha Waseme’ na hapo akafanya free style ya hip hop rap na reggae vitu ambayo kwa sasa Diamond Platnumz aka ‘Lips Denda’ ndiye mssanii maarufu bongo anayeimba na kurap kama alivyochana kwenye wimbo wa ‘Zigo Remix’ na ‘Fresh Remix’.

Otile hata hivyo amesema kuwa ngoma kali yaja muda si mrefu kama wiki mbili zijazo ambapo itakuwa ni collabo kubwa na msanii wa nje ya Kenya. Tazama video yake akirap live studioni kupitia hii link embeded.

>MitegoEA.