Tanzania kimenuka baada ya mtayarishaji wa muziki wa bongo kuvujisha ngoma ya msanii mkali humo na mwingine wa Nigeria.

Baada ya Diamond Platnumz kuachia video ya wimbo wake akishirikishwa na msanii wa Nigeria, Patoranking sasa imezuka taarifa mpya ya wimbo wa mkali huyo wa ‘No Kissing Baby’  kwamba alirekodi wimbo na msanii Ali Kiba.

Abby Dady
 

Abby Daddy producer nchini Tanzania amekiri kuvujisha collabo ya wasanii hao wawili bila idhini yao na kutoweka wazi maswala yaliosababisha kitendo hicho chake amabacho amekisema kuwa huenda kitamharibia biashara yake.

“Hicho kitu kitaniharibia biashara watu wataogopa kuja kwangu kufanya kazi, kuvujisha nyimbo ni hasara kubwa ka msanii, ni moja ya tatizo kubwa sana ni hasara kubwa sana kwa producer, nyimbo inapovuja halafu kukawa na mteja mwengine anataka kufanya kazi na wewe, ataogopa kwa kuwa wewe tabia yako ni kuvujisha”, alisema Abby Dady kwenye kipindi cha E-Newz ya EATV.

#MitegoEA.