Msanii wa kiki Kenya ameanza kutanua wigo kimuziki hadi kwenye soko kuu la kimataifa kwani muziki wake umekubalika Hollywood.

STL

Stella Mwangi  aka STL ambaye ni rapa mkali wa kike amekuwa kwenye game kwa muda na sasa ngoma yake ‘Big Girl’ inatumika kwenye filamu ijayo ya Hollywood.

Filamu ya msimu wa pili ya  ‘Bad Moms Christmas’ ambayo inatarajiwa kutoka Disemba mwaka huu itatumia ngoma ayke STL kama sound track katika channel ya HBO.

Ni ngoma iliyowahi kutumika kwenye filamu ya ‘Rough Night’ iliyotoka mapema mwezi Juni mwaka huu 2017 na kumfanya Stella kupata shavu kwenye soko la kimataifa kutokana na ustadi wake kwenye mashairi yake.

Hata hivyo kuna baadhi ya filamu ambazo zilitumia wimbo huo kwenye soundtrack kama ‘Save The Last Dance 2′,’American Pie Presents’, na ‘The Naked Mile’.

#MitegoEA.