Msanii mkali wa mistari kutoka Wcb Wasafi ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya BET 2017, ameachia wimbo mpya wa kuwaweka sawa watu kwenye mahusianao ya kimapenzi.

Rayvanny

Rayvanny aka ‘Mtu Mbaya’ ameachai kazi yake hio hapo jana Jumanne na sasa ndio talk of the town kwani wimbo upo kwenye playlist nyingi za media houses kibao Afrika Mashariki. Ray amezungumzia mapenzi ya uongo wakati mmwanamke anatoka na mwanaume mwingine kisa ana six pack ya kifua kwa kupiga gym na huku mwanaume wake hakikosa pesa anaibiwa penzi.

Rayvanny ni mtunzi mahiri wa mashairi kwenye nyimbo zake kwani ukiskiliza nyimbo zake zote hakuna moja kakosea mpaka hii mpya ‘Unaibiwa’. Kwa mujibu wa Ray ni kwamba  wanawake na wanaume siku hizi hakuna mapenzi ya kweli bali sifa na kutafuta wenye uwezo wa kifedha sio lakini pia wenye ‘six pack’ kifuani. Wapo wanawake watakuchanganya kwa vicheko na tabasamu za bandia. Nao wanaume wakiwa na pesa wanasifiwa vitambi na magari kumbe sio mili zao bali vitu vya kukopa tu.

“Ukiwa na pesa utasifiwa kitambi, beby i like that..na kukupamba kwenye simu, video snapchat, kumbe hana maana Mangi anamwita sweetheart, kisa ana kesha gym kutafuta six pack” anaimba Rayvanny. “Unadhani ni wa peke yako kumbe wengine wameshaweka kambi, kakupendea macho wengine kawapendea rangi, ni gari la dampo halichagui taka dereva mpe ganji..akibadili sample akila mihogo karoti hazipandi..Unaibiiwaa” kamaliza hivyo kwenye wimbo wake mpya.

Skiliza wimbo huo hapa chini;

>MitegoEA.