Msanii gwiji na mkongwe kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya amefunguka ya moyoni na kuweka wazi umri aliyowahi kiss yake ya kwanza.

Redsan ni mkali wa muziki wa dancehall ambaye anafahamika kimataifa kupitia sana yake ambayo anaiwakilisha vizuri na hivyo kumpa heshima ya hadhi yake kutokana na bidii pamoja na kukaa kwa industry kwa miaka zaidi ya kumi tangu aanze muziki.

Akiwa live Radio Maisha kwenye Konnect Show ya Mwende Macharia pamoja na Clemmo 254, ameyajibu maswali ‘Kumi Noma’ zake mtayarishaji Hassan Omar kwa kusema kuwa alianza kubusu mwanamke wa kwanza akiwa na umri wa miaka kumi na saba (17). Amesema wazi kuwa kama akipata simu kutoka kwa mrembo wake akidai anataka waongee bila shaka atawaza kuwa ana mimba yake.

Clemmo, Redsan na Mwende

Mkali huyo ameachia hit song kadhaa kama vile, Not Normal, Shika Glass, Unbreakable, Badder dan Most, Shoulder Back na sasa ametambulisha wimbo mpya kwa jina ‘Whine Fi Mi’ ambayo atifanyiavideo na kuitambulisha wiki ijayo.

Tazama kwenye hii video hapa chini;

 

>MitegoEA.