Msanii wa gospel nchini  Kenya na ambaye amekuwa na jina kubwa kutokana na juhudi zake za kuhakikisha muziki unafikia hatua ya kimataifa zaidi na kumpakulia shabiki kazi nzuri anapokuwa studioni ameeleza uhusiano wake wa kikazi na msanii Weezdom.

Bahati

Bahati ambaye kwa sasa ana miliki record label yake Eastlands Most Beloved (EMB Records) ambayo ipo kwa ajili ya kuwasaidia wasanii kufikia ndoto zao kimuziki kwani inatoa fursa kwa waanii haswa wachanga kurekodi kazi zenye ubora mkubwa. Msanii huyo akizungumza kupitia Maisha Concert Friday ndani ya Radio Maisha, amefunguka wazi kuhusu uhusaino wake wa kikazi na msanii aliyekuwa kwenye lebo hio yake kabla ya kutokea mshike mshike na kubidi ahame humo. Weezdom ni msanii wa gospel pia ambaye amejishindia tuzo kama vile Groove Awards 2017 na Mwafaka Awards 2016 japo kwa nyimbo tatu tangu aanze usanii. Amekuwa kwenye EMB Records chini ya boss wake huyo ambaye ni Bahati.

Mkali huyo wa ‘Nikumbushe’ ameiambia Radio Maisha kuwa Weezdom alikuwa akimsaidia tu wala hakuwa amejisajili rasmi kwenye lebo yake. “Unajua EMB Records hatusainishi msanii ovyo ovyo tu kuna vigezo tunazingatia sana na labda vilikosekana kwake. Mimi sikuwa nimemsaign but tu kumsaidia apate kujulikana” akasema Bahati.

Msanii Bahati amekuwa akitambulisha wimbo mpya aliyoshirikisha msanii chini ya lebo hio yake kwa jina David Wonder na ngoma inaitwa ‘Ndogo Ndogo’ kupitia Maisha Concert Friday pamoja na Nick Odhiambo na Nyosh Gathu.

> MitegoEA.