Redsan ni msanii anayefahamika kupitia muziki wake wa aina ya dancehall ambao ameufanya kwa zaidi ya maiaka kumi kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya ni mmoja wa wasanii wachache ambao hutowakuta kwenye bifu za kimuziki na wasanii wengine kwani anatambua uwezo wake na pia kuheshimu kazi yake.

Redsan

Mkali huyo wa ‘Whine Fi Me’ amezungumzia suala la wasanii kutopata shavu kwenye music label kubwa za kimataifa kwani kwa mujibu wake yeye ni kwamba wasanii wengi wanashindwa kufanya muziki wa kuachia album na kukimbilia kuachia singles ambazo hazina muda mrefu kwenye game la muziki duniani. Akizungumza na Radio Maisha kwenye Konnect show amesema hivi;

“Record labels dont sing artist doing singles but albums kwa sababu ni biashara hile na muziki wa album una soko kubwa na biashara yake iko vizuri kwani ndio zinaleta pesa vile vile kumuuza msanii ili kufahamika uwezo wake kikamilifu. Bila album hunachemsha tu” akasema Redsan.

Swabri Mohammed aka Redsan kwa sasa ana takriban album saba ambazo zipo sokoni kwa ajili ya mauzo. Msanii huyo wa Reggae, Ragga na Dancehall ameweka wazi kuhusu collabo ayke na msanii mkali wa bongo fleva, Ali Kiba mabyo waliifanya ,mwaka 2015 na mpaka sasa bado haijaachiwa.

“Yaah, kuna collabo yetu na Ali Kiba kutoka mwaka 2015 but unreleased due to copyright issues but soon itakuwa tayari” yeye kamaliza hivyo.

>MitegoEA.