Bifu la wasanii wa gospel nchini Kenya limenuka na sasa wasanii hao hawana mwelewano kama ilivyokuwa mwanzoni wakati wakiwa kwenye lebo moja ya EMB Records.

Bahati

Bahati ndiye boss wa lebo hio ya muziki maarufu kama Eastlands Most Beloved, ambapo anafanyia kazi zake za muziki lakini pia kuwapa nafasi wasanii wengine kutumia studio hio kurekodia ngoma zao kibiashara.

Juzi Bahati amezungumzia uhusiano wake kimuziki na msanii aliyekuwa kwenye lebo hio, Weezdom. Kwa mujibu wake alisema kuwa akuwa amemsainisha msanii huyo wa ‘Testify’ kweny EMB Records bali alikuwa tu akimpa usaidizi pekee kama msanii mdogo ili apate kujulikana. Akizungumza kwenye Radio Maisha Bahati alifunguka hayo kitu ambacho alikikana msanii Weezdom.

Weezdom

Weezdom amepiga gumzo na Mitego Sasa Blog na kubainisha hali halisi ya uhusiano wao. Kwanza ameanza na kusema kuwa maneno ya Bahati kuhusu kumsaidia kimziki ni ‘Utoto tu’ na sio kwamba alikuwa akipata usaidizi kwenye lebo hio kwani alikuwa amesainishwa rasmi kwenye lebo hio.

“We dont need to contest about that..its all over YouTube my first interviews zote nilikuwa na yeye akinitambulisha kwa media as the first signed” yeye kamaliza hivyo.

#MitegoEA.