Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Diamond asikitikia hatua ya yeye kuamua kumlipia Hamisa gharama ya maisha wakati yupo mjamzito kwa mtoto ambaye amekiri wazi ni wake baada ya vita ya maneno mitandaoni.

Simba ameeleza kero ya kuona pesa zake zikitumika kulipa watu kumtukana na kumchafulia jina pamoja na familia yake kutokana na ujauzito wa Hamisa Mobetto.

Hamisa Mobetto

“Nilikuwa natoa zile hela (Laki 5/wiki) lakini tena zile hela zikawa zinalipwa watu mitandaoni wanitukana” afunguka Platnumz wakati akizungumza na kito kimoja cha habari, Clouds FM Tanzania.

Hata hivyo baada ya kuweka wazi kuhusu mtoto kuwa ni damu yake hajakataa kama akimwanika kwenye mitandao ya kijamii kama afanyavyo kwa watoto wake na Zari pamoja na yeye mwenyewe.

“Hata baadae ninaweza kumposti, nina picha zake ..Mimi naamini ni mtoto wa kwangu” akaongeza kusema kuwa, Siwezi kumchukia Hamisa, ila namshauri muda huu aangalie future ya mtoto, kwani kuposti picha mitandaoni haitamsaidia”.

Hatimaye amemaliza kwa kusema kama Zari naye kipata mtoto wa nje ya ndoa sio tatizo bora maelewano tu.

Zari akichepuka utamsamehe? “Ni maisha ya kawaida cha msingi ni kujua mstakabali wa maisha yenu” yeye kamaliza hivyo Platnumz.

 

Diamond na Zari

#MitegoEA.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.