Msanii wa kike wa Kenya ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha sanaa ya muziki Kenya imepiga hatua nyingine ya kimataifa zaidi kutokana na harakati zake za kusukuma muziki mzuri duniani.

Muthoni Drummer Queen (MDQ) ni rapa mkali kwenye mashairi yake na amefunguka mengi kuhusu kupambana na hali halisi ya muziki kama msanii wa kike anayefahamu malengo na changamoto za kazi ya muziki. MDQ kupitia Radio Maisha kwenye Konnect Show, amekiri wazi kuwa  wasanii wengi hawaheshimiwi kutokana na hali zao za kutosimama kwenye mstari wa mbele kuonyesha wachokifanya kimasomaso bila kuhofia lolote kwani muziki ni sawa na ofisi yoyote ile.

Wasanii wengi hajafahamu uwezo wao ndio maana hawana heshima kwenye jamii na mashabiki wao, wanatakiwa kusimama kimasomamaso kubaini kazi zao. Mimi MDQ najielewa ndio maana najituma mno kufikia malengo ya muziki wangu” akasema MDQ.

MDQ

Mwanamuziki huyo ambaye pia ni balozi wa kinywaji cha Belaire Champagne, ameshafanya ngoma kibao na watayarishaji muziki wakubwa duniani lakini pia kupiga tamasha za kuzindua na kuhamasisha wasanii kwenye kanda ya Afrika Mashariki. ” Nimepiga show nchini Uganda, Rwanda, Burundi tukifanya motisha ya wanamuziki East Afrika na kupitia campaign hio nimejifunza mengi na kujuana na watu maaraufu kwenye game la muziki” akasema msanii huyo.

Hata hivyo, kwenye kitengo cha masawali kumi noma, amefunguka kwamba yeye anaweza kukubali Khaligraph Jones kumbebea handbag wala sio msanii Timmy Tdat. Ameweka wazi yeye ni bora kuwa na mwanaume anayeota na kuongea usingizini kuliko kuwa na nightwalker.

“Yaa ni bora chali anaye-sleep talk kuliko sleep walk coz anaweza kutoka nje ya nyumba uchi usiku na kuniaibisha au kushukiwa mchawi” akamaliza hivyo MDQ.

MDQ kwa sasa anatamba na ngoma mpya ‘Million Voice’ baada ya ‘Kenyan Message’ na ameahidi kuachia album yake mwezi Novemba mwaka huu.

>MitegoEA.