Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Katika harakati za kupambana na kulifunua soko la muziki na tasnia ya muziki nchini Kenya, Mitego Sasa Blog imekita kambi Pwani ya Mombasa Kenya kunako chimbo la madini ya muziki mzuri ambao hujafumbuliwa.

Vijana wengi ukanda huo wa pwani wamejaaliwa kuwa na uwezo mkubwa wa kukutengenezea furaha  kupitia sanaa yao ya muziki licha ya tuhuma na skendo za kujihusisha na mihadarati.

Snomey

Msanii Snomey Lee ni mmoja wa wasanii ibuka a Pwani ya Kenya ambaye pamoja na kujitahidi kukithi mahaitaji ya familia yake, anapambana kuhakikisha talanta yake ya muziki imetimia. Kwenye umri wake wa miaka 30, Snomey msanii wa hip hop ameachia ngoma mbili kwa jina ‘Nataka‘ na ‘Vuka Border’.

Ni msanii lakini pia anafanya kazi ya kinyozi ili kujiongeza na kujipatia kipato huku akiamini siku yake itatimia na kuwa bonge la staa kimuziki.

Ngoma yake ya kwanza ‘Nataka’ imetayarishwa na  Mchafuzi kwenye Crack Sound Records huku wi,mbo wa pili, ‘Vuka Border’ ukitayarishwa na Noizer Pan De Beat kwenye  Green House Production japo collabo na msanii Ti Maitsi.

Snomey kwa sasa anatarajia kuachia ngoma nyingine ya gospel kwa jina ‘You Are My Everything Jesus‘ kwenye Blue Moon Records. Ngoma zeke zipi kwenye YouTube na SoundCloud.

Tazama wimbo wake ‘Vuka Border’ hapa chini;

#MitegoSasa.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.