Msanii wa nyimbo za injili Kenya amebainisha wazi kuwa mtindo wa muziki wake sasa ni wa kidunia wala sio gospel tena. Msanii huyo ambaye kwa sasa amechukua headlines kupitia ngoma yake mpya kwa jina ‘Jigi Jigi’ amekuwa gumzo kutokana na kubadilika kwa mfumo wa aina ya muziki anaoimba.

Willy Paul aka Pozee na sifa kwenye tasnia ya muziki japo wapo baadhi ya watu wasioelewa ni mtindo gani wa muziki wake japo yeye anadai ni style ya gospel bongo. Wasanii wameanza kulegeza kamba kwenye utunzi wa mashairi ya kumsifu Mungu au labda ni mtindo mpya wa kuchanganya mambo ya dunia kwenye utumishi wa mmbo ya kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mkali huyo wa Jigi Jigi’ ameachia ngoma kadhaa zenye ladha ya bongo fleva zenye ujumbe mzito wa kimapenzi kwa mwanawake na kuwaaminisha mashabiki kwamba ni muziki wa gopsel japo maana ya neno ‘Jigi Jigi’ ni kumaanisha tendo la ngono kitandani. Willy Poze ameonekana kwenye picha na baadhi ya mashabiki wake huku akipost kwenye Facebook yake kuwa kampa mmoja wao Jaketi yake apige picha nayo kama shabimi wa ‘Jigi Jigi’.

“Yesterday I gave my #jigijigi fan my jacket apige nayo picha coz she liked it… thank you for ur support my people” alipost Pozee

MitegoEA.