Msanii wa kike na ambaye hajakomaa kwenye game la muziki japo mtangazaji maarufu wa televisheni nchini Kenya, amejitokeza na kuweka wazi ya moyoni kuhusu lebo moja ya muziki Kenya.

Mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma zake kama vile ‘Give it to you’ amesema kwenye kipindi cha Maisha Concert Friday Radio Maisha kuwa alipokuwa chini ya lebo ya muziki ya Kaka Empire hakufaidika chochote hadi mwenyewe kujitoa humo kwani aliona kama anajipotezea muda.Kumbuka pia msanii wa bongo fleva, Rich Mavoko aliondoka kwenywe record lebo hio na kujiunga na Wcb Wasafi yake Diamond Platnumz Tanzania.

Chess Nthusi

“I was like what im I doing here coz everything mine was stagnant, so mimi nikaona bora nijitoe Kaka Empire” akasema Chess.

Ni mtangazaji mahiri kwani alishafanya vipindi vya Tv kama cha Y-Connect kwenye Ebru Tv lakini kuondoka humo baada ya alichokisema kuwa kampuni ilifilisika ghafla na hivyo kuamua kuendeleza kipaji chake cha muziki. Chess kwa sasa ana collabo mpya audio ‘Vumilia’ bado video akishirikiana na rapper Prezzo baada ya kazi yao ya pamoja ‘Celebration of Life’ alipata shavu kutoka kwa mkali huyo baada ya kuskia sauti yake na ubunifu wake hivyo kumtafuta aingize chorus ya ngoma hio.

Hata hivyo licha ya kuwa msanii mchanga kwenye tasnia ya muziki, amebahatika kutajwa kuwania tuzo za AFRIMA 2017 huko Nigeria mwezi Novemba tarehe 12 kwenye kipengele cha Best Female Artist In Eastern Africa kupitia ngoma yake ‘Give It To You’.

Amewaomba mashabiki wote wa muziki kumpigia kura ili ailete tuzo hio nyimbani kwani ameteuliwa kwenye kitengo hicho pamoja na wasanii wengine wakali kama vile Victoria Kimani ambaye amemtaja kama msanii mkubwa kwake lakini pia role model wake kimuziki.uUnaweza kumpigia kura yako kwa kubonyeza hii link> www.Afrima.com Tazma hio video kisha usikose kubonyeza Subscribe!!

>MitegoEA.