Muziki wa nchini Kenya unazidi kupamba moto na kuboreshwa na nguvu mpya za vijana wenye nguvu na ujuzi kwenye fani hii ya sanaa ya muziki kusaidia jamii.

Mitego Sasa Blog imekusogezea msanii chipukizi anayejiamini mno kupitia kazi yake ya kurekodi muziki studioni japo kakumbana na changamoto nyingi hadi kufikia hatua ya kurekodi ngoma yake hii ya kwanza kwa jina ‘Throne‘ kwani alitengwa na marafiki ila akapata usaidizi wa familia yake iliyosimama naye kipindi hicho hadi leo.

“I had the passion for music since i was young i have been many problems through this journey there were many critic with my friend only my family stood for me but i thank God for being here” akadokeza Leon Kariuki.

Leon Kariuki

Leon Kariuki ni msanii mwenye bidii na malengo makubwa maishani kwenye umri wake mchanga wa miaka 18 na sasa video ya ngoma hio ipo tayari kwenye YouTube channel yake. Ameshirikisha msanii Chacha Zawadi.

 video ‘Throne’ hii hapa chini;

#MitegoEA