Beryl Owano ni mwanamziki mahiri anayetesa anga  kwa kibao chake kipya ‘Slowly’ aliyomshirikisha mkali wa bongo fleva  Matonya kutoka nchi jirani ya Tanzania.

Amefunguka alipokuwa akihojiwa kwenye Radio station moja nchini, kuhusiana na issue nzima ya collabo hiyo. Ilkuwa inadaiwa kuwa alimlipa Matonya wakafanya ile collabo, “Nina nyimbo nyingi studion na huwa nawatumia top Djs nyimbo zangu kabla sijazitoa ili nipate mtazamo wao. Wimbo wangu “slowly” nilikuwa nimeufanya na nikamtumia Dj ambaye kwa bahati nzuri alikuwa na matonya, alipoicheza wimbo huwa,Matonya aliupenda sana ndiposa akanipigia na kuniomba collabo”akasema Berly.

MATONYA KAMKATIA BERYL  OWANO??

Berly na Matonya

Kwa mara nyingi wanadada wanaojitosa kwenye biashara ya muziki hulalama kuwa wananyanyaswa kimapenzi. Hali hii si tofauti na anayopitia msanii Beryl Owano.

Amesema kuwa anapitia wakati mgumu hasa wakati anajaribu kuusukuma muziki wake. “Wakati mwingi nakatishwa tamaa kwa kuwa waume naokumbana nao hasa nikiwa katika harakati za kupush mziki wangu hutaka tutoke kimapenzi ndiposa wanisaidie…..lakini Matonya ni gentleman, nimeskiza nyimbo zake tokea niwe mdogo na nikatamani sana kufanya  kazi naye ……muda wote ambao nimekuwa nae hajawai nikatia ama kunishawishi nitoke nae kimapenzi kama wasani na madjs wengine.”yeye kamaliza hivyo msanii Berly Owano.

Na; G-Deal msanii.

#MitegoEA.