Mapya ya utapeli wa muziki yamebainishwa na sasa hali ni tete kwani wasanii maraufu kwa muziki nchini Kenya wanadaiwa kuiba ngoma ya wasanii chipukizi.

Wimbo ‘Wembe’ wake Timmy T Dat akishirikiana na msanii wa pwani ya Kenya, Otile Brown unapigwa kila kona ya chini na sehemu kibao za burudani lakini imeibuka kuwa sio ngoma yao kwani aliiba ngoma ya wasanii wawili wachanga kwenye game ya muziki, Spizzo na Bandanah wimbo wao kwa jina ‘Wenge’.

Mitego Sasa imepiga story na msanii wa ngoma ‘Wenge’, Spizzo Cpy na kuweka wazi kuwa ngoma yao hio japo hijavuma sana Kenya iliwagharimu pesa nyingi kwenye studio kurekodi kisha kuifanyia video maeneo ya Zanzibar na Mombasa.

“Ni ngoma yetu hio amekopy na kupesti tu kwani ‘Wenge’ ndio tu amebadilisha kuwa ‘Wembe’ but mistari na flow ni ile yetu kabisa labda waliona sisi ni sasanii wadogo ndio watuibie idea zetu” akasema Spizzo.

Hata hivyo msanii huyo amesema kuwa kuna wakati alikuwa akitaka kufanya collabo na msanii Otile lakini haikuwezekana kwa sababu Otile alimtaka amlipe kiasi cha pesa Ksh 200,000 kwa ajili ya hio collabo.

“Mimi nilimtaka Otile tufanye collabo kwenye ngoma nyinge tofauti akaniitisha pesa kibao sikuwa nauwezo, 200,000 shillings. Akanitaka nimtumie ngoma zangu askilize kama nina uwezo wa kufanya kazi na yeye nikamtumia hio ‘Wenge’ baadae akujibu kitu bali na kunambia ngoma ngoma ni kali hii” Spizzo kaendelea kusema kuwa msanii Timmy T Dat alikuja kwenye video launching ya ‘Wenge’ na baadae akawaambia ameipenda hio ngoma sana”.

Licha ya hayo, Mitego Sasa imejaribu kumfikia msanii Otile ili kubainisha madai hayo lakini hakuzungumza kitu kuhusaina na utepeli huo.

Hii hapa chini ni video fupi sampuli ya ngoma hizo mbili ‘Wenge’ na ‘Wembe’. Tazama uone kama kweli ni utapeli au la.

#MitegoEA.