Jana Septemba 27, 2017 bunge la kitaifa la Uganda liliguzwa shamba la mieleka na ngumi kwani wabunge walitofautiana kwenye mswada wa kuondoa miaka ya kugombea nafasi ya urais kwa mujibu wa katiba ya nchi hio.

Sio tu kwa majirani zetu, bali pia hali kama hio ilishawahi kushuhudiwa bungeni Kenya wakati wabunge walitandikana na kuraruriana nguo mbele ya spika wa bunge kwa tofauti za kivyama vya kisiasa ulioleta mgawanyiko hadi kusambaratisha matukio na shughuli  bungeni.

Uganda mbele ya spika Rebecca Kadaga ugomvi ulizuka na wabunge kupigana ngumi, kuharibu spika na kurushiana viti kutokana na muswada huo uliopingwa na wengi. Barani Afriaka matujkio kama hayo sio mapya kwani waafrika hutofautiana kwenye itikadi na kasumba zao wala sio kwenye hoja na kuishia kupigana makonde badala ya kutafuta suluhu la kudumu.

Somalia, Kenya vikao vya bunge vilishawahi kukatizwa kutokana na vurugu za kutoafikiana kwenye mambo ya kujali maslahi ya vyama wala sio hoja za kuleta maendeleo nchini. Afrika Kusini wanasiasa waliwahi kupigana kwenye televisheni kwa tofautiza  ya mitazamo ya vyama husika vya kisiasa.

>MitegoEA.