Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Muziki umekuwa na mabadiliko mengi yanayoleta uchangamfu wa sanaa lakini pia kutia changamoto kwa kila msanii. Wasanii wengi wemekuwa wakijiunga makundi au bendi ili kufanikisha kazi nzuri zenye adhi ya kimataifa zaidi na kuwafikia mashabiki wao kwa urahisi.

Afrika Mashariki kuna makundi ya muziki kama vile Yamoto bendi ya Tanzania, High Pitch Band ya Kenya, Sauti Sol, H_Art The Band, Kelele Takatifu miongoni mwa nyinginezo. Africa Magharaibi kuna Psquare na kitu cha ajabu ni kuwa makundi mengi yameanza kusambaratika.

Moji

Baada ya taarifa kuhusu Yamoto Bendi kutolewa na msanii meneja Mh. Temba na kusema wazi kuwa watu wenye mali na pesa ndio wanaharibu muziki wa mabendi kama walivyofanya Yamoto kwa kugawa wasanii ili kila mmoja ajitegemee, sasa hali kama hio imetokea nchini Kenya kwenye kundi la wasanii wa gospel maaraufu kama Kelele Takatifu.

Kundi hilo linahusisha msanii Moji Short Baba na Didi lakini baada ya taarifa kuhusu kusambaratika kwa kundi, Moji ameweka bayana kuwa bado Kelele Takatifu ingalipo japo kila msanii kwa sasa anakitahidi kufanya kazi kivyake kama bibla inavyozungumzia nyakati za kufanya kazi.

“Kelele Takatifu bado ipo sana but now kila msanii anafanya solo projects ndio maana sisi bado tupo kwenye group yetu na hatuwezi fanya kama wanavyofanya wasanii wengine kwenye bendi zao. Sama tu ni swala la wakati na bible imesema kuwa kuna wakati wa kila kitu na huu ndio wakati kila msanii  wa Kelele Takatifu anafanya solo projects” akasema Moji.

Kumbuka Psquare walisambaratika na sasa Peter na Paul kina mmoja ni  msanii kivyake licha ya kuwa ni mapacha. Moji Short Baba amezindua ngoma yake mpya ‘Kuzitoka’ ndani ya Maisha Concert Friday, Radio Maisha na Nick Odhimbo na Alex Mwakideu.

>MitegoEA.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.