Simba wa madale aka Diamond Platnumz amepagawisha kwenye siku yake muhimu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huku akifurahia siku hio kwa siku tatu mfululizo.

Picha: MillardAyo

Baada ya siku muhimu ya mpenzi wake Diamond, Zari Hassan kusherehekea siku yake ya kuzaliwa juzi mwezi Septemba huko Afrika Kusini, kisha ikafuatia birthday party yake Ex-Girlfriend wake Diamond, Wema Sepetu mwishoni mwa mwezi Sepetemba, sasa imekuwa zamu ya msanii na kipenzi chao, Diamond aka Chibu Dangote.

Msanii huyo amejiachia na kusherekea siku yake hio kuanzia mapema Ijumaa, Jumamosi, Jumapili kisha siku yake rasmi Jumatatu tarehe 2, Oktoba 2017 siku aliyozaliwa. Diamond amealika marafiki wake mashuhuri kwenye house party yake na miongoni mwao ni aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Jacqueline Wolper ana ambaye alishatoka kimapenzi na msanii nchini ya Wcb Wasafi, Harmonize.

Picha: MillardAyo

Kwenye sherehe hio ya kipekee iliyofanyika maeneo tofauti kuanzia Element Club Masaki Dar Es Salaam, kwenye mashua na pia kwenye jumba la mkali huyo wa ngoma ‘Hallelujah‘, kipenzi chake cha hivi karibuni Hamisa Mobetto na manye kwa sasa ana mtoto pamoja na Diamond, Dyllan hakuwachwa nyuma kwenye birthdat party ya mpenzi wake huyo mpya.

Picha;MillardAyo

Timu zima ya Wcb Wasfi kuanzia usimamizi, wasanii chini ya lebo hio, madansa na pia wana mitindo mbalimbali mbali walihusika kwenye birthday ya Platnumz.

Picha: MillardAyo

Warembo kibao na wanamitindo wa aina ayke Tanzania walijirusha kwenye bonge la sherehe hizo za Platnumz lakini cha ajabu ni kuwa mzazi mwenzake Diamond, Zari Hassan hakutokea kwenye Party ya mpenzi wake licha ya Diamond kuhudhuria sherehe ya siku yake ya kuzaliwa juzi huko South Africa. Kwenye ujumbe wake alisema bado yeye anashughuli huko nchini Afrika Kusini.

Manager Sallam aka Mendez. Picha:MillardAyo
Diamond akiimba ngoma yake ‘Hallelujah’. Picha: MillardAyo