Mkali wa rap nchi Kenya amefunguka kuhusu remix ya ngoma yake ‘Tippy Toe’ aliyowashirikisha wasanii wengi wakali Kenya.

Femi One

Femi One aliachia collabo hio pamoja na msanii Kristoff aka Mluhya wa Busia na baada ya kutesa anga za muziki na burudani, amerudi kuirudia kwa mtindo tofauti akijumuisha wali wa muziki. Femi ni msanii aliyechini ya studio za kurekodi ngoma za Kaka Empire. Amewashirikisha wasanii Fena Gitu, DJ JR, Timmy Tdat, Kristoff na CEO wa Kaka Empire, Kaka Empire.

Msanii huyo akipiga gumzo na kituo kimoja cha media bongo Tanzania amefunguka na kusema haya; “Nimefarijika sana kwa kufanya kazi na wasanii hawa wakubwa kwenye remix hii.” Femi One asema.

“Nimejifunza mengi kutoka kwa kazi zao. Ninajivunia kwa Fena Gitu na Timmy Tdat ambao wamependekezwa. Kristoff ni genius kwa kuusikia muziki mzuri na uwezo wa King Kaka wa kukaa kwenye muziki wowote ni mkubwa,” akasema Femi One.

Tazama video hio mpya hapa chini;

>MitegoEA.