Mkali wa dancehall nchini Kenya ameachia ngoma na video mpya inayosumbua kwenye media mbalimbali kwa sasa kutokana utamu wa kazi hio licha ya kuwa ni gwiji wa mistari na mashairi makali.

Wyre

Wyre aka The Love Child amekuwa maarufu kupitia kazi zake za sanaa kama vile ‘Nakupenda Pia ft Alaine, Kingstone Girl, Usaba wa Uongo, Njoo Nami’ miongoni mwa nyinginezo. Ni msanii wa Nairobi Kenya ambaye amekuwa gumzo siku za hapo nyuma ila kwa sasa amerudi na ujio mpyabada ya ukimya wake kwenye game la muziki.

Chini ya producer Ivan Odie na director M.S.Y.O.X (Eric Musyoka), Wyre ameachia ngoma hio mpya kwa jina ‘Number’ huku akizungumzia kuishiwa na subira ya kuongea na mrembo wake na sasa naomba apewe hio namba ya simu ili kuonegesha mahaba kupitia mongezi ya simu.

Tazama video yake hapa chini.

>MitegoEA.