Nchini Tanzania kumekuwa na msururu wa sherehe za siku za kuzaliwa kwa sanaii wengi humo waliopo chini ya lebo moja ya muziki maarufu kama Wcb Wasafi Records ambapo wasanii watatu wameadhimisha siku hio muhimu.

Baada ya Sherehe ya boss wa Wcb Wasafi, Diamond Platnumz kukamilika tarehe 2 Oktoba, ailifuatia ya msanii  Harmonize pamoja na Marombosso. Kumbuka Zari mpenzi wake Platnumz hakuhudhuria sherehe za siku ya mzazi mwenzake Diamond kwa kisingizio kuwa yuko bize nchi Afrika Kusini kwenye miradi ya biashara zake. Hata hivyo Hamisa Mobetto mzazi mpya mwenzake Diamond alikuwepo kwenye maadhimisho hayo.

Harmonize kissing Sarah: Picha; Dizzim Online

Kwenye siku ya mkali wa ‘Happy Birthday’, Harmonize alionekana akila denda la mpenzi wake mpya kutokea nchini Italy mbele ya umati wakati wakilishana keki ya siku ya kuzaliwa kwa Harmonize. Sarah ndilo jina lake mrembo huyo ambaye kwa sasa ana mimba ya msanii huyo na huenda akajifungua hivi karibuni. Kumbuka Harmonize naye alimteam mpenzi wake wa awali, Jacqueline Wolper mwigijazi wa filamu bongo na kumwendea Sarah, lakini walikutana macho kwa macho kwa mara ya kwanza baad aya kuachana kwenye birthday party ya Diamond ndani ya jumba lake Simba.

Harmonize alioneka kuhofia kumlisha mpenzi wake Sarah keki mbele ya watu lakini aliishia kumlisha na kumpa bonge la busu huku wakiburudika na ngoma hio ya ‘Happy Birthday’ iliyokuwa ikiimbwa na msanii Lava Lava.

>MitegoEA