Msanii gwiji wa muziki wa bongo fleva nchini Tanzania bado anazidi kudhihirisha kwamba bado yupo ngangari kinoma kwenye utunzi wa mashairi makali ya kuvutia yenye ladha tele ya kimapenzi.

Ni msanii wa kike wa kitambo kwenye game la muziki ambaye ameachia rekodi kubwa ya muziki kwa kurekodi album kibao huku akipiga hit song nyingi kama vile ‘Yahaya, Ndindindi, Joto Hasira, Siku Hazigandi’ na nyinginezo.

Lady Jay Dee

Lady Jay Dee aka Judith Wambura Mbibo mkali wa R&B bongo, ameachia ngoma mpya sasa na video ipo tayari kwenye mitandao ya kijamii kama vile YouTube channel yake. Ngoma kwa jina ‘I Miss You’ inazungumzia hisia za kweli anazokuwa nazo mtu anapokuwa amempeza mpenzi wake kwa muda.

Audio imetayrishwa na Man Water wa Tanzania huku video yake ikiongozwa na mkali kutoka Afrika Kusini, Justin Campos. Itazame hii hapa chini;

>MitegoEA.