Unapenda muziki mzuri na kufurahia kuwa mmoja wenye timu za muziki na wafuasi wa wasanii? Basi usikose hii hapa inakuhusu kutoka kwa wasanii wawili wa Kenya ambao wamehusika kwenye collabo kwenye ngoma yao mpya lakini pia kuachia album.

Clemmo, Bobby Mapesa, Mwende na Calvo

BC yaani Bobby Mapesa na Calvo Mistari kupitia Konnect Radio Maisha wametambulisha ngoma yao mpya ‘Murder’ waliyowapa shavu ‘H_The Band kundi la muziki nchini Kenya. Wawili hao wakiwa Live studioni wamesema kuwa wao sio kundi bali ni wasanii kila mmoja anajisimamiana kupambana na kazi zake lakini wanashauriana na kufanay kazi za pamoja.

“Sisi  ni indivindual artists but tuanakuwa pamoja na tuanfanya kazi za pamoja tunapota time” wasanii hao wameongezea kusema kuwa muzki wa album unalipa kwa wasanii wanaotambua uwezo wao na wenye majina makubwa tu.

“Muziki wa album unalipa na una soko kubwa kwa wasanii wenye majina makubwa sio wasiojulikana kwenye game au wanawafuasi wachache kwenye mitandao. Sisi ndio wasanii wanaofanya album pekee” akajigamba Calvo Mistari.

Kwenye album hio yao mpya inajumuisha ngoma kumi na nne (14) walizorekodi kwa kipindi cha miezi sita kwa mujibu wao huku wakiwashirikisha wasanii wengine wakali wa nje na ndani ya nchi yetu.

“Tumeshirikisha wasanii kadhaa kama vile Fena Gitu, Dela, H_The Band, Petra na msanii wa bongo, Mr Blue” akasema Bobby Mapesa.

Album yao itazinduliwa kesho rasmi ambapo wasanii kadhaa watakuwepo kwenye ukumbi huo kama vile King Kaka, Avril, Sauti Sol,Fena, Dela, H_The Band, Femi One na wengineo kibao. Kiingilio ni miguu yako.

Calvo, Mkazivae na Bobby Mapesa

>MitegoEA.