Dah! Kimenuka maeneo ya mitandaoni kwenye akaunti za watu na wapenzi wenye majina maarufu wenye wafuasi wengi kutokana na hali ya kutoelewana kwenye mahusiano yao hivi karibuni.

Zari

Diamond Platnumz ni mzazi mwenzake Zari Hassan ambaye pia ni mfanya biashara Afrika Kusini lakini kufuatia hatua ya msanii huyo wa bongo fleva kutangaza wazi kuwa alitoka kimapenzi na video vixen,Hamisa Mobetto na kubahatia kupata mtoto pamoja kwa jina Dyallan, sasa imezua kashfa na taharuki mitandaoni kwani Diamond ameshafuta picha zote za mpenzi wake Zari kwenye mtandao wa Instagram na kubakisha moja tu ya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa. Zari naye hakumwacha salama Diamond kwani pia aliishia kuzifuta zote za Diamond, Wcb Wasafi, watoto wake Nillan na Tiffah pamoja na za famila ya Diamond na watu wengine wa Tanzania.

Mitandaoni kumekuwa na maneno na mabo kibao kuhusu suala hilo la kudhilishana mbele ya mashabiki wao huku watu wafuasi wao wakifunguka ya moyoni na kuingilia mahusiano hayo ya Zari na Diamond. Diamond a;ihudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Zari huko Afrika Kusini lakini Zari hakuonekana kwenye birthday party ya ‘Simba wa Madale’ Platnumz kwa kisingizio kwamba ana shughuli nyingi maishani.

Hata hivyo kufuatia kusambaratika kwa mawasiliano ya wapenzi hao wawili, kumeonyesha faraja kwa aliyekuwa mpenzi wake wa awali, Wema Sepetu na mashabiki wake kwani wemekuwa mstari wa mbele kuchangia moto kwenye ugomvi huyo wa Zari na Diamond kisa yeye ameanza mapenzi na mrembo wa bongo Tanzania, Mobetto na inadaiwa kuwa Zari alimchongea Wema kwenye penzi la Platnumz.

Picha: Dizzim Online

Pichani ni Diamond akimlisha keki mrembo wa msanii wa Wcb Harmonize kwenye birthday party ya Harmonize nyumbani kwa msanii huyo wa Kimakonde. Mrembo huyo kwa jina Saraha kutoka Italy ana mimba ya Harmonize na huenda akajifungua siku za karibuni.

>MitegoEA.

1 COMMENT

Comments are closed.