Msanii wa gospel kenya anafahamika mwa mitindo mipya ya kudensi na ngoma kali kali zenye ujumbe maalum amerudi kuachia ngoma mpya na densi mpya.

Bruz Newton

Bruz Newton ametambulisha ujio wake huo mpya ‘Witinesi’ kupitia Maisha Concert Friday na kufunguka wazi kuhusu miradi ya kazi zake zijazo na wasanii wapya kwenye game la muziki. Bruz aka Nwewton Mwangi amekiri wazi kuwa alisaidiwa pakubwa kupata jina na kufahamika kwenye muziki na msanii Collins Manjale ‘Collo’ kupitia ngoma yao ya pamoja ‘Bazokizo‘ anbayo inapendwa na kila rika kwani watu uimba na kuicheza bila hofu.

Msanii huyo kwa sasa anatamba na ngoma hio mpya ambayo imetayarishwa na msanii producer, Jegede huku ‘Bazokizo na Zikwembe’ zikitayarishwa na Jack on the Beat. Bruz amefunguka kusema kuwa haina zote za densi kwenye ngoma zake huwa anashirikisha wenzake ambao ni madansa ili kubuni aina nzuri na ya kipekee kucheza kwenye kila ngoma wanapoachia video.

Bruz Newton

Kupitia Radio Maisha mkali huyo wa ‘Zikwembe’ amesema kuwa amefanya collabo nyingi na wasanii wapya kwenye tasnia ya muziki huku kazi hizo zikitayarishwa na producer Jack.

>MitegoEA