Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Diamond Platnumz aliachia ngoma hapo awali kwa jina ‘Utanipenda‘ na kwenye ujumbe wa wimbo huo anauliza mpenzi wake Zari kama akifilisaka kose pesa atampenda bado na kwenye vido anaonekana mrembo huyo akiitikia kutoamuacha hata kwa hali gani.

Diamond Picha; Wasafi studios

Juzi vurugu za kimapenzi kati ya Diamond na mrembo huyo mzazi mwenzake zimeibuka na kutikisa mitandao kwa kinachodaiwa kuwa Platnumz aka baba Tiffah na Nillan anatoka kimapenzi na Hamisa Mobetto. Habari za mitaaani na mitandaoni zimedhihirisha wazi kuwa wawili hao hapo kwenye mahusiano mema kwa sasa huku cheche za dharau na matusi zikitawala.

Baada ya wapenzi hao futana picha zao kwenye Instagram account zao, Diamond ameishia kupost akisema kuwa yeye hayupo kwenye mahusiano na mwanamke yeyote na kwamba angali mchanga kuingia kwenye ndoa kwa sasa kwani ndio mwanzo ametimiza miaka 28 juzi ameadhimisha sherehe za siku yake muhimu ya kuzaliwa Oktoba 2,2017.

Alichokipost Diamond

Simba amezungumza na kusema kuwa hata akianza kuoa anaruhusiwa kuoa wake zaidi ya wanne kulingana na dini yake ya Kiislam. Ameongeza kuwa anajitahidi kupeleka muziki wa bongo fleva kwenye soko la dunia kwa hivo hataki mambo ya kimapenzi au watu kusafiria nyota yake na kiki za bure.

>MitegoEA.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.