Penzi limechina na sasa imebakia kiporo tena wanasema waswahili kuwa linanuka baada ya kuzuka kwa choko choko kwenye mahusiano ya Diamond Platnumz na Zari Hassan mzazi mwenzake.

Diamond na Mobetto

Msanii huyo wa bongo fleva amekuwa gumzo kila pembe na sasa inaonekana maji ya shingo yanamwendesha mbio kutokana na mahusiano yake mapya na video viex wa bongo, Hamisa Mobetto aliye na mtoto wa msanii huyo anaitwa Dyllan.

Baada ya Hamisa kujifungua mtoto huyo alianza kumsuta msanii huyo huku akionekana kutaka kumdhalilisha au labda kusafiria nyota ya Diamond ili ajizolee sifa kibao mitandaoni. Alianza kwa kudai kuwa Diamond anadhalilisha na pia kutelekeza mtoto wao kwani anaseam kuwa hajali huyo mtoto  na hivyo kumfikisha mahakamani kumfungulia kesi.

Licha ya Mobetto kuteuliwa kwenye tuzo mbili huko Afrika Kusini, inadaiwa kuwa pia Diamond alimpa gari jipya alilokusudia kumpa mama yake mzazi kama zawadi na hivyo kuna fununu kuwa mama yake Diamond alikasirishwa na kitendo hicho cha Hamisa kumilikishwa zawadi yake wakati akijifungua mtoto huyo wa Platnumz. Kwenye barua hio iliotoka kwa mahakama imeandikwa kuwa ‘Take Note the above named case has been set for 30/10/2017 at 7:30′. Kesi ni mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba saa moja unusu.

Hata hivyo baada ya Zari kufuta picha za Diamond na familia yake lakini pia za watu wa Tanzania kwenye Instagram yake, aibuka na jipya kusema kuwa pia mtoto wa pili wake (Nillan) sio damu ayke Diamond licha ya vipimo vya awali vya DNA. Je hii ni Movie au ni Uzushii?

>MitegoEA.