Diamond Platnumz alishuka jiji la Kampala mwishoni mwa wiki jana tarehe 6 Oktoba 2017 kwa ajili ya kutoa bonge la burudani kwa mashabiki wake na pia kusaidia kuchangisha pesa ili wanafunzi kunufaika na eleimu bora.

Mkali huyo wa muziki wa bongo fleva alikuwa kwenye tamasha la Kampala City Festival baada ya yeye kupaa angani kwa ndege kuhudhuria tuzo za Afrimma 2017 huko Dallas  Texas Marekani. Diamond alifika Uganda na kupokelewa kama mfalme au ‘Simba’ na maelfu ya mashabiki waliokuwa wanamsaifia kwa muita ‘Simbaa’ huku wakikazania kusalimia mkononi na kupiga ‘Selfies’ na mkali huyo wa ngoma ‘Hallelujah’.

‘Simba’

Platnumz alipiga show kwenye Independence Grounds Kololo Kampala na kutangamana na watu mbalimbali waliofika kisha akahutumia kikao kwenye Serena Hotel Conference Center Uganda kabla ya kufululiza hadi kwenye Nakivuba Settlement Primary School. Tamasha hilo limekusudia kusaidai wanafunzi wa shule 79 za KCCA ambapo shule zinahitaji vifaa vipya vya masomo kama vile vitabu, ujenzi wa vyoo, jiko, madawati na pia mazingira bora ya kufanikisha elimu bora. Kupitia kampeni hio ya msanii Diamond, fedha hizo zilikusanywa kupitia malipo ya malngoni kuingia kwenye show ya mkali huyo wa Tanzania.

>MitegoEA.