Kumbe wapo watu ambao hula jasho lao wala hawapendi kujihusisha na mambo ya utapeli kwenye biashara zao?  Wasanii kama kioo cha jamii wanatakiwa kuwa mfano bora kwa kila mtu anayewaangalia au kuwategemea kwani wanafaa kutumia sanaa yao kuelimisha jamii.

Msanii wa gospel Kenya anayetamba na ngoma kali kama vile ‘Vidole, Check Vile’ na nyimginezo, amefunguka mengi kwenye maswali Kumi Noma ndani ya Konnect show Radio Maisha na Mwende pamoja na Clemmo.

 Eko Dydda amekuwa akitesa kwenye tasnia ya muziki wa injili na amejishindia tuzi kadhaa kama vile Groove Awards. Akiwa Lve kwenye show ya Konnect amesema kuwa yeye alishawahi kutumiwa pesa kwa bahati mbaya na mtu asiyemjua lakini hakuitumia wala kutapeli amesma kuwa alimrudishia tu.

“Mimi sikuitumia pesa hio nilimrudishia tu coz aliona jina langu na labda angepiga screenshot na kunianika kwa mitandao ya jamii kama WhatsApp” akasema Eko Dydda. Ameongeza kusema kuwa alinunuliwa nguo aliyoivaa kwenye video yake ya ‘Niko na Reason’ msanii Holy Dave.

Clemmo na Eko Dydda

Mkali kwa sasa anatamba na ngoma mpya ‘Bow’ ambayo maana yake ni kusujudu mbele za Mwenyezi Mungu kumpa shukrani na kuwapa heshima watu wakubwa na kila mtu kwa ujumla. Eko Dydda ameweka wazi kuwa watoto wake wawili (Wavulana) watakuwa wanaachia ngoma yao ya pamoja wiki ijayo. Watoto wake wanaitwa I Am Blessed na Keep It Real.

Keep It Real
I Am Blessed

Hata hivyo amefunguka  kwa kusema kuwa yeye anajipanga kuachia albamu ya mapachi wala sio ya ngoma japo kwa utani tu.

>MitegoEA.