Simba wa Madale kutoka nchini Tanzania amezidi kutanua wigo kwenye tasnia ya muziki wake na sasa amekita kambi zaidi ugaibuni pande za Marekani.

Msanii huyo wa bongo fleva amekuwa na mafanikio makubwa kwenye kazi ya sanaa yake tangu aanze muziki kwani kila siku anapiga hatua ya kumuongeza maishani. Baada ya kuachia collabo za nguvu na msanii Patoranking, Ne-Yo, Morgan Heritage sasa anadondosha bonge la collabo na msanii kubwa na mkali wa hip hop Marekani na duniani kote.

Nitaachia-albamu-ya-amapicha-sio-ya-ngoma-eko-dydda/

Diamond Rick Ross

Diamond Platnumz anazidi kung’aa kama vile jina lake kwani collabo yao imeonekana tayari wakati msanii huyo wa ‘Hallelujah’ alikutua Dallas, Marekani kwa ajili ya kupokea tuzo yake ya Best East Africa Artist kwenye tuzo za Afrimma 2017. Diamond alikuwa ameandamana na msanii chini ya lebo yake ya Wcb Wasafi na mshindi wa BET 2017, Rayvanny japo hakufanikiwa kutwaa tuzo yoyote.

Msanii huyo wa bongo fleva, Simba ameonekana kwenye picha na video inayoonyesha wakirekodi video ya collabo ya ngoma yao mpya ijayo pamoja na Rick Ross.

“Uganda wasanii wamelala sana” alalama mtangazaji wa radio

Rick Ross, Rayvanny na Diamond

Tazama video hii hapa chini uone kilichotendeka. Video kwa hisani ya BDozen.

Diamond Rick Ross

http://mitego.co.ke/2017/10/10/part-29-ile-nduru-alitoa-no-joke/

MitegoEA