Bongo Tanzania kuna watu wanapenda au wanajua kuzua utani mitandaoni kwa kazi za wenzao japo kuwapa kiki tu.

Baada ya video inayomwonyesha msanii boss wa Wcb Wasafi akiwa location na msanii mkubwa wa hip hop duniani, Rick Ross watu mbalimbali wameanza kuizungumzia kwa namna tofauti. Wasanii na watu maarufu ameonekana kusambza video hio huku mchekeshaji mshindi wa Big Brother Africa (BBA), Idris Sultan akizidisha kicheko kwa alichokiandika kwa akaunti yake ya Twitter muda mfupi baada ya teaser kuhusu video hio. Ameandika akama ifuatavyo;

“This is good news 👏🏽👏🏽 ila hapo utafikiri Ross kaja kumtuliza mdogo wake kichaa maana Mond anaruka ruka balaa au ni mimi tu nimeona ?”😆 ameandika Idris

Idris na Diamond

Idris ni mtani wa zamani rafiki yake Diamond Platnumz lakini siku za hivi karibuni kumezuka taarifa za bifu kati yao na kila mmoja humzungumzia mwenzake kwa utani mkubwa. je ni support ya kujenga sanaa au ni bifu za kuharibu kazi zao?

>MitegoEA