Je ushawahi kujikuta katika hali ngumu kama hii ambapo unatakiwa ufanye kazi fulani kisha ukaishia kufanya kinymue chake? Na je kama ishawahi kutokea, ulikabiliana na hali hio vipi?

Mchoraji huyu wa kike pichani alitakiwa kuchora Tattoo kwenye mgongo wa mwanaume huyo anayeonekana kama ni mteja wake, lakini kwa jinsi alivyoagizwa kuchora akifuata mchoro wa picha kwenye karatasi, aliishia kufanya mambo yake.

Mchoro huo wenye mfano wa farasi mwenye mabawa mwanaume huyo alikuwa anatarajia achorwe kama ilivyokuwa kwenye hio karatasi. Mwanamke huyo anaonekana kubabaika baada ya kugundua amechora visivyo kwani mchoro wake ni kama Ng’ombe au Kipepeo.

Je kama ni wewe umechora au kuchorwa vibaya hio Tattoo utachukua hatua gani?

>MitegoEA