Mwanamitindo ambaye pia ni mfanyabiashara nchini Afrika Kusini ametua nchini Tanzania na mara hii sio kumwona tena Diamond Platnumz kwani waliachana kisa kusalitiwa kimapenzi na msanii huyo wa bongo fleva.

Zarinah Hassan aka The Boss Lady aliyekuwa mpenzi wake marehemu Ivan Ssemwanga kisha Diamond Platnumz aliamua kuendelea na maisha yake punde tu alipofahamu kuwa anachezewa akili na hisia zake na ‘Simba’ aka baba Tiffah na Nillan na kwa sasa yupo kwenye biashara zake Afrika Kusini kunako na familia yake.

Zarinah

Zari ametua Tanzania leo jioni kuhudhuria uzinduzi wa duka la kuuza vifaa vya nyumba na nguo la ,Danube ambapo yeye ni balozi lakini pia Diamond. Mrembo huyo akizungumza na waandishi wa habari alipotua uwanja wa ndege wa JK Nyerere International hakuwa na mtoto wake na Diamond, Nillan na amesema kuwa hajakuja kwa ajili ya Diamond.

“Nimekuja Tanzania kama balozi wa Danube sio Diamond. Kwahiyo nashukuru kwa upendo wetu, na tuendelee kutumia bidhaa za Danube,” amesema Zari.

Hata hivyo amewaomba watu wa Tanzania kujitokeza kwenye uzinduzi huo hapo kesho kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar El Salaam.

>MitegoEA

1 COMMENT

Comments are closed.