Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Kimenuka na mambo yameanza kubainika wazi huku Wakenya mbalimbali wakionyesha misimamo yao kisiasa.

Kufuatia kubatilishwa kwa ushindi wa rais Uhuru Kenyatta na mahakama kuu inayoongozwa na jaji mkuu,David Maraga, joto la kisiasa limepanda na raia wanatoa hisia zao kuhusu uamuzi wa tume ya uchaguzi IEBC ambayo kila kukicha inazidi kupingwa kupitia maandamano kwenye miji mikuu Kenya, Nairobi, Mombasa na Kisumu.

Hata hivyo IEBC inazidi kujiandaa kuendesha uchaguzi mpya au marudio tarehe 26/10/2017 kwa mujibu wa katiba ya Kenya lakini kupitia kwa WhatsApp group yao baadhi ya waliojaza nafasi za kazi kusaidia zoezi hilo wameanza kujiuzulu. 

Haya hapa maongezi kati ya IEBC na mteuliwa mmoja kwenye nafasi ya afisa msimamizi wa kituo Cha kupigia kura Isiolo. Tazama.

#MitegoEA

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.