Msanii wa gospel nchini Kenya ambaye anatamba kwa hits kibao kama ‘Niko Salama, Nimeshinda, Hainaga Makosa’ miongoni mwa nyinginezo, ameachia ngoma mpya sasa na ndio habari ya mitandaoni.

KimDanny

Kim Danny msanii wa injili amekuwa kimpya kwa muda lakini sasa amekiri wazi kuwa amerudi kwa kishindo kwenye game la muziki kwani alikuwa chuoni kusomea kozi ya Information Technology ambapo amehitimu na sasa yupo tayari kuwajibikia muziki vilivyo kwani ndicho kipaji chake.

Akizungumza kupitia Konnect show ya Mwende na Clemmo Radio Maisha, ameweka wazi kuwa tayari anafanya collabo na wasanii mbalimbali wa Afrika Mashariki.  “Nimeshafanya ngoma na msanii wa Tanzania, Uganda na sasa nataka kuachia album mpya” akasema Kim Danny.

Msanii huyo wa ‘Tulia’ ameongezea kusema kuwa ataachia collabo na msanii wa secular muziki yaani muziki wa kidunia ili kuwafikia mashabiki wote kwa ujumla kwani muziki haubagui wala hauchagui bora una ujumbe muhimu kwa msikilizaji.

Kim

Kim Danny amezindua ngoma yake mpya tayari kwa jina ‘Ajabu’ na audio imeandaliwa na Cah Centi na video chini yake Steve Hunter. Tazama video yake mpya yake hii hapa chini kisha interview yake hapo juu;

>MitegoEA