Mitego Sasa inazidi kufumbua vipaji vipya vya wasanii wachanga Afrika Mashariki na sasa imetega na kukusogezea habari kuhusus huyu msanii.

Felix 254 aka Felix Muema, amezaliwa mwaka 1998 mtaa wa Kalolenina kukulia Dagoretti Nairobi. Kwa sasa msanii huyo anakaa mataa wa Ogata Rongai anakofanyia mishe mishe zake za kupambana na maisha laini pia kuskuma muziki wake duniani.

Ni msanii wa muziki wa muhimiza wafausi wake na mashabiki kwa ujumla ila ana uwezo wa kufanya aina nyingi za muziki akam vile, bongo fleva, dancehall na hip hop.Alirekodi ngoma yake ya kwanza ndani ya Samic records mwaka 2016 na sasa ana ngoma mbili ‘Siku Njema na One Day’. Tazama video ya ngoma ayke mpya ‘One Day’ aliyowapa shavu wasanii JSaviour na Chongo Bwoy hapa chini;

>MitegoEA