Mashindano ya kuwakilisha mataifa duniani kwenye tuzo za Miss Universe tayari wateule wapo tayari kuwakilisha nchi zao na kupeperusha bendera za taifa husika kimataifa zaidi.

Wanamitindo mbalimbali wamefuzu kuwania tuzo hizo zitakazo fanyika November huko Sanya nchini China mwaka huu. Washindani wengi kutoka Afrika Mashariki waligombea nafasi hio ila hawa ndio waliobahatika kufaulu kwenye Miss World 2017.

Julitha Kabete

 

Nchini Tanzania Julitha Kabete ateuliwa na kamati kuwakilisha nchi hiyo kwenye shindano hilo mwaka huu. Julitha amewahi kuwa Miss Africa Tanzania 2016, Climate Change Ambassador.

Kenya inawakilishwa na mrembo mwanamitindo kutoka kaunti ya Elgeyo Markwet anayefahamika kwa jina Magline Jeruto atakaye peperusha bendera la taifa letu kimataifa zaidi tarehe 18/11/2017 huko Sanya Arena China.

Magline Jeruto

>MitegoEA