Dah! Inakera sana kuskia visa mbalimbali kuhusu wizi wa polisi kwa raia wa Kenya.

Baadhi ya polisi wa utawala na wale wa Kenya Police wamegeuza cheo chao kuwa sehemu kuu ya kitega uchumi. Wizi wa kuaminika wapodhulumu raia wazalendo na kuwanyima riziki yao.

Mitego Sasa Blog imefumbua vitendo hivyo vya uroho na uibilisi vya polisi wanyonge wa utawala wasiopenda kuchoka kisa mazoea ya kudoea pesa za hongo pale River Road Nairobi.

Wanawapa ulinzi wanake malaya wanaoshirikiana nao kunyanyasa wanaume kingono huku wakiwakamata na kutaka hongo kisa wanaume kuonekana na hao vitega uchumi malaya.

Picha; Mfano wa maafisa hao wezi

Kwa namna hio, polisi hao wanadharau kazi zao na kudunisha heshima ya amiri jeshi mkuu ambaye ni raisi wa Kenya na ofisi yake kwani yeye ndiye mkuu wao.

Polisi hao wameonekana kutoheshimu kazi zao kwa kusaka pesa za rahisi mifukoni mwa wanafunzi na watu wasio na hatia na kuwatishia kuwafikisha Central Police wasipopewa hongo.

Imefika wakati raia wazalendo Kenya kusimama kwa sauti moja na kutetea haki zao kwani wasiopenda maendeleo wapo na wanafanya wawezalo kuhujumu uchumi wetu wakiwemo hao polisi matapeli wanyonge wapenda vya bwerere River Road Nairobi.

#MitegoEA.

Vote MITEGO SASA as the best Blog in Xtreem Awards 2017. SMS RRA2 to 22275. Vote many times as possible, Share too!!