Dah! Haya nayo ni makubwa jamani eti  Zari ameshobokea Ali Kiba baada ya kusuasua kwa mahusiano yake na Simba Diamond Platnumz kwa sababu ya yeye kuonyesha mapenzi kwa Hamisa Mobetto.

Zari The Boss Lady mfanyabiashara mkubwa South Africa amedaiwa kutoroka na watoto wake na mzazi mwenzake Platnumz na kwa sasa haijawekwa sawa alipo. Mrembo huyo amedaiwa kumsifia mkali wa ‘Seduce Me’ Ali Kiba kupitia kituo kimoja cha radio nchini Tanzania kwa kusema kuwa Kiba anamweshimu sana lakini pia anampenda kwa misingi ambayo hakuiweka wazi.

Diamond kwa upande wake hajafunguka chochote huenda Simba ameguswa pabaya ukizingatia yeye na Ali Kiba hawapo sawa kwenye suala la muziki na mahusiano. Je Kiba atamtoa Zari kwa Simba?

Kiba na Simba

>MitegoEA