Maisha ya kufeki yapo kwa wengi duniani ila kwa hawa ni basi na kama vipo huna budi kulifuatilia hili kwa kina kama ni mpenzi wa msanii huyu chipukizi mwenye mitindo yake.

Utaskia bongo Tanzania Harmonize ametoka kimapenzi labda na msanii mwigizaji wa bongo movie, Jacqualin Wolper au binti mrembo kutoka Italy. Diamond Platnumz uliskia alishadate Wema Sepetu na kwa sasa anatamba na mwanamitindo mfanyabiashara nchini South Africa, Zarina Hassan, msanii wa muziki wa hip hop bongo, Dogo Janja naye kafunga ndoa na mwigizaji filamu bongo, Irene Woya lakini huyu hapa chipukizi msanii mtunzi matata kutoka Kenya mabaye amezimika kwake msanii mkongwe na mrembo Avril.

Mkali huyo wa ‘Show Dem, Ruka Debe na Luck Boy’ amefunguka ya moyoni kusema kuwa hakuna siku inakwisha bila yeye kumwaza mwanadada msanii huyo amabye kwa kauli yake anadai anampasua kichwa kwa mawazo na hisia za mapenzi yake.

Senior Rhymes amekuwa msanii chipukizi wa kwanza kuweka wazi kuwa napenda sana kuingia mahusiano na msanii au madada mkubwa kiumri kwani anafahamu kuwa kuna mengi ya kujifunza akiwa na mwanamke mpevu kimawazo huku akusisitizia kumtaka kimapenzi Avril.
“Wajua msanii Avril ni msanii anajielewa sana ni mrembo pia anajituma sana kufanikisha mambo mazuri kwake na pia mimi siwezi mind kiwa naye kimapenzi, namweshimu pia sana” Senior Rhymes kamaliza hivyo!

Je unadhani ni vizuri kwa msanii au mwanaume kutoka kimapenzi na mwanamke mwenye umri mkubwa kuliko yeye?
>MitegoEA