Msanii wa kike ambaye kwa sasa anatamba na ngoma kama ‘Charm’ amefunguka na kusema yaliyomsibu kipindi cha nyuma wakati alipokuwa mapenizni na mwanaume mmoja.

Vivian Wambui

Vivian Kenya amesema kuwa alikuwa akipigwa mno na kufukuzwa kwa nyumba na huyo mwanaume ambaye amesema ni ‘fala’ na kuishia kuleta mwanamke mwingine ndani.

“The idiot would beat me up, throw me out of his house after bringing in other girls. He once angrily kicked me out of his car. He called me ‘loose’ when I decided to move on and look for happiness.” amesema kupitia kituo kimoja cha runinga nchini.

Vivian amesema kuwa mateso hayo ya mwaka 2015 ndio yalichangia kupata idea ya ngoma yake mpya ‘Chingichanga’ atakayo itambulisha rasmi Monday November 6.

Kwa sasa mrembo huyo yupo kwenye mahusiano na mfanyabiashara mmiliki wa radio huko Nakuru, Sam West ambaye walikutan mara ya kwanza kupitia show ya Citizen Tv, 10/10.

>MitegoEA