Msanii wengi bongo fleva imekuwa Jambo la kawaida kutoka kimapenzi na wanawake wakubwa kiumri. 

Juzi msanii Baraka Da Prince ametangaza kuvunjika kwa mahusiano yake ya mapenzi na mrembo msanii lakini pia mwanamitindo, Najma ambaye wamedumu kwa mapenzi kwa muda mrefu.

Licha ya hayo msanii wa hip hop bongo Dogo Janja amefanikiwa kufunga ndoa na mwigizaji mmoja wa bongo movie, Irene Uwoya ambaye pia ni mkubwa kiumri zaidi ya Dogo Janja. 

Dogo Janja na Irene Uwoyao

Hata hivyo Janjaro ameweka wazi kuwa amefanya ndoa na mwanamke huyo kutokana na kuwa ni mrembo anyejiheshimu na ana sifa za kuwa mke wake.
“Irene ni mwanamke mzuri mbali na maisha ya ustaa ana heshima na ndio maana namweka ndani” Dogo Janja kafunguka.

Pia msanii huyo ameongeza kusema kuwa hataki kuzini na hivyo ameamua kuoa ili atulie kwenye ndoa na familia yake.

Mitego Sasa Blog inakutakia maisha mema kwenye ndoa yako Dogo Janja.

#MitegoEA.

1 COMMENT

Comments are closed.