Diamond Platnumz leo amefunguka na kumpa moyo mwanadada mwigizaji wa filamu bongo.

Elizabeth Michal aka Lulu ni mwigizaji wa filamu bongo ambaye anakabiliwa na shutuma za kuhusika na kifo cha gwiji mwigizaji mwenzake marehemu Steven Charles Kanumba ambaye alifariki miaka ya nyuma kwa njia za kutatanisha.
Mkali huyo wa bongo movie alidaiwa kuwa kwenye mahusiano ya mapenzi na Lulu.

Kwa sasa anaendeleza kuskiliza mashtaka yake hayo kwenye mahakama za Tanzania akisubiria hatima yake dhidi ya mauwaji yasioyo ya kukusudia ‘Man Slaughter’.

Lulu

Diamond Platnumz leo ametumia ujumbe wa kumpa moyo mrembo huyo wakati huu mgumu huku alimwambia kuwa ni mtihani tu kutoka kwa mungu na anaamini kuwa anauwezo wa kuukabili huo mtihani hivyo asitie wasiwasi.
#MitegoEA