Msanii wa gospel Kenya ametamba hadi nchini Afrika Kusini kufanya mapya.

Papa Dennis amekuwa nchini South Africa kufanya shoot ya nyimbo zake mbili chini ya lebo kubwa ya Godfather production ambapo anajivunia kuwa chini ya lebo hio maarufu duniani.
Msanii huyo yupo na usimamizi wake wa muziki pia kutoka Kenya, Maliza Umaskini ambapo ndio anafanya shughuli nyingi zake za muziki.

“Nimekuwa chini ya Godfather production tangu nianze muziki lakini pia nina management yangu yaitwa Maliza Umaskini”  yeye kamaliza hivyo.

Papa Dennis na Mr. Flavour

Hata hivyo mkali huyo  wa ‘Lokolo Dance’ amefanikiwa kupata shavu kutoka kwa msanii wa Nigeria, Mr. Flavour ambaye ameshirikiana naye kwenye kazi mpya ‘Mayaya’ ambayo kwa mujibu wake Papa Dennis ina maana ya kusifu.
Mitego Sasa imepiga story na Papa na kufunguka haya; “Nilipomcheck Mr.Flavour ili tufanye collabo hio alifurahi sana kwani alijua pia atafaidi kitu kutokana na soko la muziki na kuvuta mashabiki wa gospel music lakini pia East Africa music fans” akasema Papa.

Papa Dennis anaamini kufanya collabo na msanii wa secular kunasaidia kuvuta mashabiki wa kila upande.

Audio imetayarishwa na  Teddy pamoja na producer wa msanii Justin Beiber. Video chini ya Godfather production.
#MitegoEA.