Balaa imemkuta tena msanii ambaye kwa sasa ni mbunge wa Starehe.

Charles Njagua Kanyi aka Jaguar amehusika kwenye ajali ya barabarani maeneo ya Juja wakati wa msafara wake wa magari akitokea nyumbani kwenda jijini Nairobi.

Jaguar ambaye alikuwa kwenye gari tofauti na lililopata ajali, amenusurika ajali hiyo kwenye barabara ya Thika Highway ambapo walioumia ni walinzi wake wawili na dereva.
Gari hilo aina ya Marcedes Kompressor liligongana na gari lingine lilokuwa mbele kwenye barabara hio na majeruhi hao wamelazwa Kenyatta Hospital kwa ajili ya matibabu.

#MitegoEA

Leave a Coment