Christian Bella aka Obama msanii wa kizazi kipya kuchukua uraia wa Tanzania.

Mkali huyo wa nyimbo kibao za mtindo wa bongo fleva ni mkongoman yaani raia mzawa wa DRC Congo lakini anafanyia muziki wake bongo Tanzania.

Christian Bella

Bella kupitia Bongo Fleva Top 20 na mtangazaji Juma Jr huko Tanzania kipindi cha Jumamosi, alifunguka kuhusu suala la kubadilisha uraia kuwa Mtanzania.

“Ni kweli mimi ni kama Mtanzania kwa kuwa nimekaa bongo tangu 2005 wakati nilianza muziki wa bongo fleva na nimepata mashabiki wengi bongo kuliko kwetu Congo na hata nimekuwa niitwa na marais wa mihula mbalimbali Tanzania kwenye ufunguzi wa matukio na warsha kubwa Tanzania kutumbuiza kuliko wasanii wote hapa bongo” yeye kasema hayo.

Hata hivyo msanii huyo ameweka sawa kuwa atajiskia poa kama akiwahi uraia wa nchi hiyo kwani imemtoa kimuziki na mambo kibao.
“Bado sijapata cheti cha urai wa Tanzania lakini nitashughulikia, nitafurahi kuwa mtanzania” kamaliza hivyo Bella aka Obama!
#MitegoEA

Leave a Coment