Kutoka bongo Tanzania ni story kubwa kuhusu kaka wawili wasanii wakubwa.

Ali Kiba

Ali Kiba na Abdu Kiba nindugu wa tumbo moja ambao wanafanya muziki wa bongo fleva huku Ali akiwa ndiye mkubwa wa Abdu.
Ali Kiba amekuwa akimpa shavu sana mdogo wake huyo kimuziki ili kukua kimuziki na walishafanya collabo kama ‘Kidela, Kajiinamia’ na nyinginezo. Wawili hao hata hivyo wanategemea kuachia ngoma mpya siku ya kesho Alhamisi.

Abdu Kiba anamshirikisha kaka yake kwenye wimbo mpya kwa jina ‘Single’ ambayo video ipo chini ya director Hanscana.

Wimbo huo utakuwa wa kwanza chini ya lebo ya Kings Music ya Ali Kiba. Pia ni ngoma yake ya pili Ali mwaka huu tangu aachia ‘Seduce Me’.
Hata hivyo leo ni siku yake ya kuzaliwa Ali Kiba ambapo Radio Citizen kipindi chake Mzazi M Tuva ‘Mambo Mseto’ amempigia simu kumuwish.

#MitegoEA.

Leave a Coment