Kutoka bongo ni ujio mpya wa kazi tamu kutoka kwa record lebo mpya ya msanii Ali Kiba.

Abdu na Ali Kiba

King Kiba amefanya ya kwake baada ya ukimya tangu mtani wake Diamond Platnumz kuzindua lebo yake ya Wasafi Records.
Msanii huyo wa bongo fleva baada ya siku yake ya kuzaliwa kuadhimisha hapo Jana, Ali Kiba ametambulisha wasanii chini ya lebo yake mpya ‘Kings Music’.

Abdu Kiba  aka Single jina aliompa Ali wakati wakiwa wadogo, amesajiliwa chini ya lebo hio mpya huku akiwa wameshafanya collabo pamoja ngoma inaitwa ‘Single’ baada ya ‘Kidela’ yao kufanya vyema.

Kings Music imesainisha wasanii wanne mpaka sasa akiwemo Ali Kiba ambaye pia yupo chini ya RockStar 4000 lakini pia Sony Music.
“Nipo chini ya lebo ya kaka yangu lakini pia nina uhuru wa kufanya kazi zangu bila pressure yoyote ile. Chini ya Kings Music tupo wasanii wanne na hii nyimbo ndio collabo yetu ya pili na kakaangu Ali. Pia ataweza kunishirikisha kwenye project yake ” amenyoosha maelezo Abdu Kiba kupitia Planet Bongo EA Radio.

#MitegoEA

Leave a Coment