Ngoma kali kutoka Usafini na duniani kote imetua kinoma noma.

Diamond Platnmuz aka Simba amemshirikisha mkali wa Hip Hop wa duniani kutoka Marekani Rick Ross kwenye bonge la ngoma ‘Waka’.

Simba amekuwa America kwa kipindi kwa ajili ya kuhangaikia muziki wake. Baada ya habari kuwa collabo hio ingechelewa kidogo kuzagaa, hatimaye wakali hao wameachia mzigo.

Wawili hao ni mabalozi wa pombe ya asili ya Ufaransa japo imetengenezewa Marekani ‘Luc Belaire Champegne’. Ni ngoma ya kufanyia mauzo au marketing bidhaa hio mpya sokoni.

Tazama hapa chini;


#MitegoEA

Leave a Coment